Friday 8 September 2017

Alichokisema Rais Magufuli,kikwete,Zitto kabwe kuhusu ishu ya kupigwa risasi Mbunge Tundu Lissu.

Image result for tundu lissu apigwa risasi
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Kigoma Mjini wameungana na mamia ya Watanzania ambao wanamuombe Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye amepigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake.



"Mungu Baba uliyeahidi kuipenda Tanzania na Watoto wako, timiza Upendo wako. Mjalie Kaka yetu Lissu afya na uzima.amina" aliandika Mbunge Ridhiwani Kikwete 

Watanzania wengi wameonyesha kuguswa na kulaani kitendo hicho alichofanyiwa mbunge huyo huku wengi wao wakimuombea aweze kupata afya njema na kupona, kwa upande wa Zitto Kabwe amewataka watanzania kila mmoja kwa imani yake kumuombea kiongozi huyo ili aweze kupona. 

"Tumwombee Tundu Lissu. Kila mtu aombe kwa imani yake. Mungu ampe nafuu Inshallah" Aliandika Zitto Kabwe 


"Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka. Vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hilo la kinyama na kuwafikisha katika mikono ya sheria", ameandika Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment