Sunday 3 September 2017

Bi Mwenda Kuzikwa Leo.

Image result for magdalena sakaya
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, Magdalena Sakayaamesema chama hicho kimepokea kwa masikitiko kifo cha Mbunge mteule wa Viti Maalum Hindu Mwenda.

Hindu alifariki dunia ghafla juzi nyumbani kwake Kibada Kigamboni na anatarajiwa kuzikwa leo saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu wilayani Ilala,  Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza, jana Jumamosi Septemba 2 Sakaya amesema  Hindu alikuwa ni mpambanaji  na mtu mwenye kukijenga chama hicho  kuanzia miaka ya 90  hivyo ni pigo kubwa kuondoka kwake.
Bi Hindu Mwenda enzi za uhai wake.

‘’Hata ukifika  Tabora leo hii hakuna mwanachama wa CUF asiyemjua Hindu’ ’amesema Sakaya.

“Sijui niseme nini maana zilikuwa zimebaki siku chache tu aende Dodoma kuapishwa baada ya kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mwezi uliopita,” amesema Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua Tabora.

No comments:

Post a Comment