Wednesday, 20 September 2017

Cannavaro awarudisha Mazoezini Yanga Baada ya mazungumzo juu ya Mgomo.

Related image
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amezungumza na wachezaji wenzake kuhusiana na suala lao la kugoma.

Cannavaro, amezungumza na wachezaji wenzake kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, muda mchache kabla ya kuanza mazoezi.

Wakati akizungumza na wachezaji hao, tayari benchi la ufundi likiongozwa na Kocha George Lwandamina lilikuwa limeanza kufanya mazungumzo na wachezaji hao ambao jana waligoma kufanya mazoezi wakitaka kulipwa mishahara yao ya miezi miwili.


Baada ya mazungumzo hayo yaliyoanza takribani saa 3:30 asubuhi, hatimaye wachezaji wa Yanga walirejea kazini na kuanza mazoezi saa 3:47.

Walifanya mazoezi kwa takribani saa moja ana ushee na taarifa zinaeleza kuwa wameahidiwa suala lao kushughulikiwa.

Hivi karibuni, Cannavaro alikutana na Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Yusuf Manji aliyekuwa katika mahakama ya Kisutu na kuzungumza naye kwa muda, kitendo kilichozua gumzo kubwa.

No comments:

Post a Comment