Tuesday, 19 September 2017

Emmanuel Okwi atoa kauli yake kuhusu Kiatu cha Dhahabu.

Image result for emmanuel okwi simba
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amesema suala la kupata kiatu cha dhahabu badala yake ni kuisaidia timu yake kupata mafanikio na ikiwezekana kubeba ubingwa.

Okwi amesema suala la kiaru cha dhahabu litafuatia baada ya mafanikio ya kikosi.

“Kwanza kufanya vizuri kama timu, nataka kuisaidia timu yangu. Nashukuru tunashirikiana vizuri kama timu.

“Kama suala la kiatu cha dhahabu litatokea wakati napambana kuisaidia timu, ni jambo zuri kabisa,” alisema.


Tayari Okwi ana mabao 6 katika mechi 2 alizoichezea Simba baada ya kufunga mabao manne katika mechi ya kwanza dhidi ya Ruvu Shooting na mawili wakati Simba ikiitwanga Mwadui FC mabao 3-0.

No comments:

Post a Comment