Friday, 22 September 2017

Haji Manara aweka sawa kuhusu sare ya Simba na Mbao FC.

Image result for haji Manara
Pamoja na Simba kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mbao FC, Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema mapambano bado yanaendelea.

Manara ameonyesha kutokuwa na hofu na sare waliyipata dhidi ya Mbao FC jana, amesisitiza Simba itaendelea kupambana.

"Simba haijapoteza, tumepata sare na mapambano bado yanaendelea," alisema.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wa Yanga wamekuwa wakimtania kwamba Simba iliponea chupuchupu.

Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jana, Simba walipoteza nafasi nyingi za kufunga mabao.


No comments:

Post a Comment