Friday, 1 September 2017

HIVI PUNDE:Mahakama yafuta matokeo ya uchaguzi wa urais Kenya.

Presidential election court case: what you need to know
Mahakama ya Juu nchini Kenya imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi uliopita na kuagiza uchaguzi mpya ufanyike katika kipindi cha siku 60.

Majaji wa mahakama hiyo walisema uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi ambazo ziliathiri matokeo hayo.
Uamuzi huo wa umeifanya Kenya kuwa nchi ya kwanza Afrika ambapo upinzani umewasilisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais na wakafanikiwa.
Mgombea urais wa muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa), waziri mkuu wa zamani Raila Odinga, aliyekuwa amewasilisha kesi ya kupinga matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ameutaja uamuzi huo wa mahakama kuwa wa kihistoria.
"Leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya na kwa Afrika. Kwa mara ya kwanza, Mahakama imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais," amesema.
"Tulisema tangu awali kwamba safari yetu ya Canaan haiwezi kuzuiwa. Siku ya tarehe 8 Agosti tulivuka mto Jordan."

Bw Odinga amesema upinzani hauna imani kwamba tume ya sasa ilivyo inaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki.


Jaji Mkuu David Maraga ameagiza uchaguzi wa urais uliofanyika 8 Agosti, 2017, haukuandaliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, hivyo matokeo yake ni batili.

"Natangaza hapa kwamba Bw Kenyatta hakuchaguliwa na kutangazwa kwa njia inayofaa.
"Agizo linatolewa, kuagiza Tume ya Uchaguzi kuandaa na kufanyisha uchaguzi mwingine kwa kufuata katiba na sheria katika kipindi cha siku 60."


Muhtasari


  1. Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi
  2.  wa uchaguzi huo akiwa na kura 8,203,290 
  3. (54.27%)

  4. Tume ya uchaguzi ilisema Raila Odinga 
  5. alipata kura 6,762,224 (44.74%)

No comments:

Post a Comment