Thursday 7 September 2017

Idadi ya Mawaziri waliojiuzulu mpaka sasa Baaada ya Rais Magufuli kupokea ripoti ya madini hii leo.

Image result for rais magufuli ikulu
Baada ya Rais Magufuli leo Septemba 7, 2017 kuwataka baadhi ya viongozi ambao wametajwa kwenye ripoti za madini ya Almasi na Tanzanite kuachia nafazi zao ili kutoa nafasi kwa vyombo vya usalama kufanya kazi yake,baadhi ya mawaziri wameanza kutekeleza.


Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Ndg George Simbachawene amefunguka na kusema  alikuwa anasikiliza ripoti hiyo ya kamati ya spika na kisha baada ya kusikiliza atazungumza nini atafanya baada ya hapo huku Naibu Waziri wa Ujenzi, Edwin Ngonyani amesema anaandika barua kwa Rais Magufuli kujiuzulu wadhifa wake huo leo hii.
Edwin Ngonyani amesema hawezi kuongeza chochote katika kauli hiyo ya Rais Magufuli bali anachofanya wakati huu ni kuandika barua kwake kujiuzulu nafasi yake hiyo kama Naibu Waziri wa Ujenzi.

Hata hivyo wapo viongozi wengine wa serikali katika nafasi mbalimbali wakiwepo pia baadhi ya waliokuwa Mawaziri katika serikali ya awamu ya tano na serikali ya awamu ya nne ambao Rais Magufuli ameagiza kuwa vyombo vya usalama vifanye kazi yake ikiwezekana kuwakamata hata leo.

No comments:

Post a Comment