Saturday 2 September 2017

Kocha wa Taifa Stars Salum Mayanga atoa yake kuelekea mchezo wa leo na Botswana.

Image result for Salum Mayanga
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Botswana, leo Jumamosi zinapambana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki.

Mchezo huo ni wa kufuata Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa). Timu zote zinautumia mchezo huo kama maandalizi ya mechi zao za kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).

Katika mchezo huo, mwamuzi wa kati anatarajiwa kuwa Elly Sasii akisaidiwa na Soud Lillah (Line 1) na Frank Komba (Line 2) wakati mwamuzi wa akiba (Forth Official) atakuwa Israel Nkongo.

 Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga, alisema: “Kikosi chetu kipo tayari kwa mchezo huu ambao kwetu
ni muhimu kwa maana mbili, moja ni kujiandaa na michezo ijayo ya kufuzu Afcon, lakini pili ni kutafuta nafasi ya kupanda kwenye viwango vya Fifa.

“Kikubwa Watanzania wajitokeze uwanjani kutusapoti kwani vijana wamenihakikishia kwamba wana uwezo wa kushinda mchezo huu.”

Kwa upande wake Kocha wa Botswana, Major David Bright, alisema: “Tumekuja lakini bado tuna uchovu wa safari, lakini tunatarajia kuwa na mchezo mzuri dhidi ya Tanzania kwani hii si mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana.

“Nimepewa kikosi hiki hivi karibuni, lakini nimejaribu kuchukua wachezaji wale wazoefu na naamini tutafanya vizuri. Mechi hii ni kipimo kwetu kwa ajili ya kujiandaa na mechi za kufuzu Afcon.”

No comments:

Post a Comment