Monday, 25 September 2017

Mambo muhimu ya kuyafaham katika maisha yako ya kila siku.


Image result for LIFE
Kila Mtu anaweza kuchagua maisha anayotaka kuyaishi na hakuna wa Kumzuia, Lakini baada ya kuchagua tunavyotaka Kuishi kinachofuata ni Kupata matokeo ya yale tuliyoyachagua.

Moja ya kitu kinachoweza kukuonyesha kuwa kesho utakuwa wapi ni VIPAUMBELE VYAKO.

Kipaumbele ni kitu ambacho umekipa UMUHIMU kwa WAKATI husika ZAIDI ya kitu kingine kwenye maisha yako.

Ukitaka kujua kipaumbele katika maisha yako angalia-

1.Matumizi ya MUDA wako (Leo jaribu kuangalia unatumia masaa mengi kufanya nini zaidi). 

2.Matumizi ya PESA ZAKO baada ya kutumia kwa mambo ya lazima.

3.Kitu gani huwa unatumia muda mwingi KUSOMA/KUSIKILIZA/KUANGALIA kabla haujaanza kazi zako za kila Siku au baada ya Kumaliza.

4.Watu gani huwa unatumia muda wako mwingi kuzungumza/kuchat/kukaa nao baada ya muda wako wa kazi.

Kumbuka kila unachofanya leo kinakutengeneza kuwa mtu UTAKAYEFURAHI kesho ama UTAKAYEJILAUMU kesho.


No comments:

Post a Comment