Rais John Pombe Magufuli leo Septemba 12, 2017 amemtembelea Meja Jen. Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa katika hospitali Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo Tanzania baada ya mstaafu huyo kushambuliwa risasi na watu wasiojulikana.
Matukio ya watu kushambuliwa kwa risasi nchini yanazidi kuongezeka hili limekuwa ni tukio la pili kwa mwezi huu Septemba baada ya shambulizi la kwanza lililompata Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma, lakini pia Mbunge wa Mtama Nape Nnauye aliwahi kutishiwa bastola na watu wasiojulikana.
No comments:
Post a Comment