Tuesday, 12 September 2017

Sababu ya Zitto Kabwe na Kubenea kuitwa kuhojiwa.

Image result for zitto kabwe na kubebea
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai, amewataka wabunge Zitto Kabwe na Saed Kubenea, kufika kwenye Kamati ya Maadili ya Madaraka ya Bunge kwa ajili ya mahojiano, kutokana na taarifa walizozitoa.


Taarifa hiyo imetolewa leo bungeni wakati wa vikao vya bunge, ambapo Mbunge Zitto Kabwe anatakiwa kwenye kamati hiyo kutokana na kauli yake aliyoitoa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Spika wa Bunge kutopeleka taarifa za kamati za madini ya Almasi na Tanzania kuzijadili Bungeni.

Naye mbunge wa Ubungo Saed Kubenea anahitajika kutokana na kauli yake aliyotoa kanisani kuhusu tukio la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu.

No comments:

Post a Comment