Mabeyo amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kudai kuwa kwa sasa wanataka kujiridhisha kuwa silaha hizo zinazotumika na hao wahalifu zinatoka wapi na watu hao wasiojulikana ni watu wa aina gani, hivyo amewataka wananchi kuviachia vyombo vya ulinzi na usalama vifanye kazi yake.
"Haya matukio tunaendelea kukabiliana nayo kama yale matukio ya Kibiti, kwanini matukio ya Kibiti hayaleti mshtuko mkubwa sana sasa wakati watu waliothirika ni wengi zaidi kuliko matukio ya sasa? Mimi sitaki kuingia huko lakini nasema vyombo vya ulinzi na usalama wakati wote vinakabiliana na matukio kadili yanavyojitokeza na ninaamini hali itakuwa shwali na sasa vinashughulika, hoja ya msingi tunataka kujiridhisha silaha hizi zinatoka wapi? Hawa watu ni wa aina gani sasa vyombo mviachie vifanye kazi yake msitoa majibu haraka" alisisitiza Mabeyo
No comments:
Post a Comment