Friday, 22 September 2017

Wizkid aandika recodi mpya ya kuandikwa katika Guinness The Book of Record.

Image result for wizkid and drake
Mwanamuziki wa Kinigeria mwenye jina kubwa Afrika, anayekimbiza kila kona, Wizkid ameweka rekodi mpya ya kuwekwa katika Kitabu cha Rekodi za Dunia, Guinness The Book of Record kwa kuweka rekodi ambayo haikuwahi kuwekwa hapo kabla.


na siku ya  jana rasmi jamaa alifanikiwa kuandikwa katika kitabu hicho baada ya wimbo wake alioimba na Drake, One Dance kupigwa katika mitandao mingi ukiwemo Spotify.
Japokuwa mtandao huo haupo nchini Nigeria lakini watu wengi wameupakua kwa wingi huku ukishika nafasi za juu katika chati mbalimbali duniani kitu ambacho tangu dunia ilipoumbwa, kitu kama hicho hakikuwahi kutokea kwa wanamuziki wa barani Afrika.
Kumbuka kuwa wimbo huo ulichaguliwa kuwa wimbo bora wa mwaka kwa Apple Music,wimbo wa tano kwa kuuzwa sana nchini Marekani na rekodi kibao ambazo kwa uswahilini tungesema ameshindwa kuzibeba kwa jinsi zilivyokuwa nyingi.
Image result for wizkid in guinness book of record

No comments:

Post a Comment