Tuesday, 31 October 2017

Baada ya Lazaro Nyalandu kuomba nafasi CHADEMA Freeman Mbowe atoa maneno yake.

Image result for Freeman Mbowe akiwa na waandishi wa habari
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Aikael Mbowe, amemkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM , Lazaro Nyalandu baada ya kuweka wazi matamanio yake wapi pa kwenda baada ya kujiuzulu.

 Mwenyekiti Mbowe ametoa fursa ya kumkaribisha ndani ya chama hicho Mhe. Nyalandu kupitia ukurasa wake wa Twitter na kumwambia kuwa hata masuala aliyoyaibua yalikuwa ni ajenda ya chama chao kwa muda mrefu.

"Milango iko wazi kwako Lazaro Nyalandu  kujiunga na CHADEMA. Masuala uliyoyaibua yamekuwa ajenda yetu kuu kwa muda mrefu"ameandika Mh. Mbowe.

Mh. Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM jana  alitangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile alichodai kwamba hafurahishwi na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama wataridhia wampe nafasi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kupitia chama hicho.
Milango iko wazi kwako @LazaroNyalandu kujiunga na CHADEMA. Masuala uliyoyaibua yamekuwa ajenda yetu kuu kwa muda mrefu.

Advertisement

No comments:

Post a Comment