Tuesday, 31 October 2017

Yanga FC yaendelea kujipanga dhidi ya Singida United wafanya mazoezi ya Mwendokasi.



Baada ya kufanya mazoezi ya gym jana, Yanga leo imeanza mazoezi ya uwanjani kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Singida United.


Timu hizo, zinatarajiwa kuvaana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Namfua Mkoani Singida katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Yanga jana chini ya Kocha Mkuu wa timu hiyo Mzambia, George Lwandamina alionekana akikiandaa kikosi hicho kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku akiwapa mbinu mbalimbali.
Katika mazoezi hiyo, walikosekana wachezaji majeruhi Mrundi, Amissi Tambwe na Wazimbabwe, Thabani Kamusoko na Donald Ngoma.

Akizungumza maandalizi hayo, Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema maandalizi ya kikosio hicho kwa ajili ya mchezo dhidi ya Singida yanakwenda vizuri katika kuhakikisha wanapata pointi tatu muhimu.

“Kama unavyoona mwenyewe katika mazoezi haya, wachezaji watatu pekee ndiyo hawapo mazoezi kutokana na majeraha ambao ni Tambwe, Kamusoko na Tambwe ndiyo pekee huenda wakaikosa mechi hii.
“Lakini wachezaji wengine wote wapo fiti na timu inatarajiwa kusafiri kuelekea Singida kesho kutwa Alhamisi,”alisema Saleh.
mwisho

No comments:

Post a Comment