Zile dalili kwamba sasa haiwezekani kwa kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko kuiuchezea Yanga dhidi ya Simba Jumamosi zimetimia.
Kamusoko ambaye alikuwa anatibiwa jijini Dar esa Salaam, ameshindwa kujiunga na kambi ya Yanga iliyo mjini Morogoro.
Yanga imepiga kambi mjini Morogoro kujiandaa na mechi hiyo ya kesho huku Kocha Mkuu George Lwandamina anaonekana ameishajipanga kivingine.
kuwaondoa kwenye mipango yake.
Juhudi kubwa zilifanywa kuonekana Kamusoko anacheza ikiwa ni pamoja na kumpumzisha ili apone haraka lakini inaonekana kuna ugumu.
Hadi jana saa 4 asubuhi hakuwa ameingia kambini Yanga, maana yake hawezi kuwa nafasi ya kucheza.
Awali ilielezwa alikuwa akifanya mazoezi jijini Dar es Salaam lakini Yanga leo itafanya mazoezi ya mwisho na kama atajiunga na kikosi leo bado hatakuwa na nafasi ya kuanza.
No comments:
Post a Comment