Thursday 26 October 2017

Mambo ya hatari ya kuyaepuka katika maisha ya kila siku.


Related image
Disorganised life(Kukosa mpangilio) 
Kuna Watu kila siku akiamka asubuhi anatumia dakika 20 kutafuta nguo ya Kuvaa, kuna mwingine leo amehangaika kutafuta Ufunguo wa gari kwa sababu Jana alisahau aliuweka wapi,au haujawahi kusikia mtu anatumia dakika 15 kutafuta soksi ya pili kwa sababu zote alizonazo ni za mguu wa kulia? 

Kuna mwingine ofisini kwako kila siku kuna kitu amesahau alipoweka-Kila wakati utasikia anasema "Yaani Niliweka hapa Nakumbuka kabisa, sijui Nani amechukua "

Watu wa namna hii tunasema wanasumbuliwa na "Clutter Syndrome"-dalili za ugonjwa wa kutopanga mambo yao vizuri. Kama kila siku unatumia dakika 30 kutafuta vitu ambavyo hujui umeviweka wapi kwa mwaka ni kwa na dakika 10,800 ambazo ni Sawa na kupoteza wastani wa siku 8 kila mwaka. 

Kuanzia leo panga vitu yako vizuri siku kabla, Amua andaa nguo utakayovaa, panga dawati lako la kazini vizuri ama eneo lako la biashara na panga ratiba yako siku yako vizuri.

Maelekezo yasiyokamilika(incomplete instructions). 
Moja ya uwezo ambao Watu wengi wamepoteza kwa sasa ni uwezo wa kusikiliza kwa makini(attentive listening). Watu wengi siki hizi hawasikilizi ili KUELEWA ila wanasikiliza ili KUJIBU, matokeo yake wanakosa kupata taarifa muhimu wanazopewa. 

UNAPOPEWA maelekezo au UNAPOTOA maelekezo kwa mtu mwingine hakikisha yamekamilika kwa 100% kwani usipofanya hivyo Utafanya tofauti na itakulazimu kutumia muda mwingine KUREKEBISHA ulichofanya. 

Ukipewa Maelekezo na bosi wako hakikisha umeelewa vizuri, USIKURUPUKE kufanya Halafu Unakuja kuambiwa URUDIE kazi ama Unaonekana umefanya TOFAUTI. 

Unapopokea maelekezo-Hakikisha Unaandika Au unaweza kurudia kuyasema kwa aliyekupa ili kuona kama umeelewa alivyotaka ama KUULIZA swali usipoelewa. 

Usiwe Wale Watu ambao ni Waoga kupata ufafanuzi matokeo yake wanafanya ndivyo sivyo kila wakati na wanalazimika kurudia kazi. 

Kama wewe unampa maelekezo mwingine,hakikisha unatoa maelekezo yaliyojitosheleza.Kila Unapotoa maelekezo nusunusu yatakurudia na utajikuta hiyo kazi inakuchukulia muda wako zaidi. 

Ukialikwa mahali,pata maelekezo yanayojitosheleza ya agenda, muda, mahali husika n.k(Kuna mtu alishawahi kualikwa kwenye mkutano Dar Es salaam akaenda eneo la posta Kumbe mkutano ulikuwa mbezi, kisa ni kwamba hotel zilikuwa sehemu mbili zinazofanana majina yeye akaasume itakuwa ni ile anayoifahamu, ilibidi atumie bodaboda ili kuwahi). Siku zote kabla haujaanza kazi yoyote ile HAKIKISHA UMEELEWA VIZURI itakuokolea muda wako mwingi wa kuambiwa-"Sikumaanisha hivyo".

Kama Unatoa maelekezo usiaasume mtu ataelewa unavyotaka,bali HAKIKISHA AMEELEWA unavyotaka

Watu wanaokupumzikia(trasgressors). 

Kuna Watu ambao kama mko nao ofisi moja wakishafanya kazi zao wakimaliza muda wanapotaka kupumzika na kukusanya nguvu wanachofanya ni kuanza kutembea kwenye Meza za wengine na kupiga stori. Usipokuwa makini kila wakati watakuwa wanakutumia wewe kupumzika na wanakufanya Uache kazi zako na kuwasikiliza. Hawa huwa wanaitwa "officus interruptus"

Huwa wanapatikana maeneo ya biashara, kwenye vyombo vya usafiri na hata mashuleni. Utashangaa tu wanakuja na kukuanzishia stori hazina kichwa Wala miguu.Ukiwagundua unatakiwa usiwape hata dakika moja kwani ukiwazoesha siku ya kwanza watakuwa kila siku wanafanya hivyo. 
Wakati mwingine Watu Hawa wanaweza kuwa mbali na wewe ila wakipata ofa ya muda wa maongezi,utakuta wanakupigia simu na Wala hawana agenda ya maana, wanaanza kukuuliza "Mambo vipi","ishu zinaendaje","Mechi ulicheki jana","Vipi Barick maoni yako","Kuna jamaa tulimaliza naye unakumbuka? "kiufupi mazungumzo yao Huwa hayana hata muunganiko.Unakuta ndani ya dakika 10 kuna mambo kama 10 tofauti ameongea.

Siku hizi hata kwenye groups za Watsapp hawa utawakuta. Akifanya kazi muda wake wa kupumzika anakuja anaanza kutuma meseji na kuanzisha topics mbalimbali na anataka kila mtu achangie. Yeye ni muda wake wa kupumzika, kama wewe ni muda wako wa kazi, USIKUBALI AKUPUMZIKIE. 
Leo ukimgundua mtu huyu, Mwambie fasta "USINIPUMZIKIE"

Vikao visivyo na Ufanisi(Ineffective Meetings)
 
Taasisi ya utafiti ya Gallop iliwahi kufanya utafiti na kugundua kuwa Kadiri unavyopanda juu kimajukumu Unaweza kujikuta unatumia takribani 80% ya muda wako kwenye vikao. 

Changamoto kubwa Huwa ni kuwa vikao visivyo na ufanisi na vinavyokuchukulia muda zaidi ya ule unaotakiwa. Bila kujali vikao hivi unavifanya kwa kukutana uso kwa uso, kwa njia ya simu ama Skype, ni lazima uhakikishe unatumia muda mfupi uwezavyo. 

Moja hakikisha kila kikao kinawekewa agenda hata kama unakutana na mtu mmoja,ajenda ziwekwe wazi kabla ya kukutana. 

Mbili ni muhimu Kukubaliana muda mtakaotumia kwa ajili ya kikao Chenu na ikiwezekana kama kuna Ajenda nyingi kuwa na muda maalumu wa Kujadiliana kila Ajenda husika. 

Tatu kudhibiti Watu wanaopenda kutoka nje ya Mada. Kuna Watu Huwa wanasababisha vikao kuwa virefu kw sababu kila baada ya muda mchache Huwa wanaingiza Mada tofauti na naanza Kujadili na kuacha Mada iliyowakutanisha. Usiruhusu Kujadili Mada isiyo husika hadi mmemaliza Mada iliyowakutanisha.

Nne ni kudhibiti "attention seekers"-Hawa ni Wale ambao wanapenda kuchangia kila kipengele hata wasivyovijua vizuri ili mradi tu waonekane. Matokeo yake Huwa wanarudiarudia yale ambayo wengine wameongea.

Kumbuka MAFANIKIO YA KAZI/BIASHARA SIO VIKAO VINGI bali VIKAO VYENYE UFANISI. 

No comments:

Post a Comment