Thursday, 26 October 2017

Tetesi zote za soka kutoka barani Ulaya hii Leo.

Image result for Philippe Coutinho
Barcelona bado wanaendelea na mkakati wa kutaka kumsajili Philippe Coutinho mnamo mwezi wa Januari, huku Liverpool ikiweka thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kuwa £133m. (Mundo Deportivo - in Spanish).

Tottenham wanamsaka kiungo wa kati wa Ajax Donny van de Beek, 20, na kinda mwenye umri wa miaka 18- Justin Kluivert, mwanawe mshambuliaji wa zamani wa Uholanzi Patrick. (Sky Sports)
Marcos Reus
Image captionMarcos Reus
Arsenal na Manchester United wote wanamchunguza mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund', 28, Marco Reus, ambaye kandarasi yake inakamilika mwishoni mwa msimu huu (Sky Germany, via Daily Mail)
Newcastle na West Brom wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Wolves' ,24, Conor Coady. (Sun)
Luke Shaw na kocha Jose Mourinho
Image captionLuke Shaw na kocha Jose Mourinho
Beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw, 22, ana wasiwasi kwamba huenda asipate fursa ya kuichezea klabu hiyo baada ya uhusiano wake na meneja Jose Mourinho kuharibika. (Guardian)
Shaw na Mourinho wanadaiwa kutozungumziana kufuatia madai ya beki huyo wa kushoto kwamba hachezeshwi msimu huu. (Times)
Arsenal wanamtaka aliyekuwa mkurugenzi wa Barcelonar Raul Sanlleh
Image captionArsenal wanamtaka aliyekuwa mkurugenzi wa Barcelonar Raul Sanlleh
Arsenal wanamtaka aliyekuwa mkurugenzi wa Barcelonar Raul Sanllehi, ambaye alihusika katika kumsajili Neymar kama mkurugenzi mpya wa operesheni.(Sport - in Spanish)
Winga wa zamani wa Arsenal Marc Overmars, ambaye sasa ni mkurugenzi katika klabu ya Ajax pia ni mgombea mwengine wa wadhfa huo. (Independent)
Wamiliki wa ardhi katika uwanja wa West Ham wako katika hatari ya kufilisika , huku West Ham wakiwa katika hatari ya kufurushwa katika uwanja huo. (Sun)
Mmiliki wa Arsenal Stan Kroenke
Image captionMmiliki wa Arsenal Stan Kroenke
Mmiliki wa Arsenal Stan Kroenke anasema kuwa klabu hiyo haijakufa moyo wa kuwaweka kiungo wakati Mesut Ozil, 29, na mshambuliaji Alexis Sanchez, 28. (Telegraph)
Kroenke anasema kuwa hatoiuza klabu hiyo na anapanga kuirithisha familia yake umiliki huo . (Mirror)
Wakfu wa mashabiki wa Arsenal unamtaka mwana wa Kroenke Josh na mwenyekiti wa Sir Chips Keswick kutoajiriwa katika bodi ya wakurugenzi. (Daily Mail)
Mshambuliaji wa West Ham Angelo Ogbonna
Image captionMshambuliaji wa West Ham Angelo Ogbonna
Mshambuliaji wa West Ham Angelo Ogbonna hakuamini baada ya timu hiyo kuwashangaza wachezaji wa Spurs kwa kutoka nyuma 2-0 na kubadili mambo kuwa 3-2 na hivyobasi kufuzu katika robo fainali ya kombe la Carabao.
Lakini je alisahau kwamba tayari wako katika uwanja wa Wembley.
Asamoah Gyan
Image captionAsamoah Gyan
Mshambuliaji wa zamani wa Sunderland Asamoah Gyan, 31, ambaye anaichezea klabu ya Uturuki ya Kayserispor, anatarajiwa kuanzisha kampuni yake ya ndege baada ya kupata leseni ya biashara hiyo nchini Ghana. (Sun)
Mauricio Pochettino anadai Daniel Levy hawawekei viwango vya umri wachezaji wanaosainiwa na Tottenham licha ya klabu hiyo kuwapendelea wachezaji wachanga wakati inapoingia katika soko. (London Evening Standard)
Beki wa Crystal Palace Pape Souare alibahatika baada ya tisheti yake aliowarushia mashabiki kurudishwa na shabiki aliyeipata. (Telegraph)
Arsenal na Manchester City zinaweza kulazimika kucheza mechi za marejeleo ya kombe la EFL raundi ya nne baada ya kuwatoa na kuwaingiza wachezaji wengi katika kipindi cha lala salama. (Sun)

No comments:

Post a Comment