Friday 6 October 2017

Hali ya kipa mpya wa simba sasa Said Mohamed “Nduda”.

Image result for Said Mohamed “Nduda”
Kipa mpya wa Simba, Said Mohamed “Nduda” anafanyiwa upasuaji wa goti leo mchana.

Nduda yuko nchini India ambako atafanyiwa upasuaji baada ya kutua nchini humo salama.

Nduda aliyeanza kuwika akiwa Majimaji ya Songea kabla ya kujiunga na Yanga, alitua Simba akitokea Mtibwa Sugar baada ya kucheza mechi moja ya michuano ya Cosafa na kuwa kipa bora.

Kipa huyo aliondoka nchini siku chache kwenda India kwa ajili ya kazi ya upasuaji huo.

No comments:

Post a Comment