Friday 6 October 2017

Ushauri aliopewa Rais Magufuli kuhusu Tundu Lissu.

Image result for Rais John Magufuli
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha amemshauri Rais John Magufuli kuwashauri makamanda wake wakubali msaada wa kusaidiwa uchunguzi wa matukio ya kihalifu yanayotokea nchini kwa sasa kwani msaada siyo fedheha.


Masha amesema hayo akiwa kwenye mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na wanahabari, leo mchana na kusema kwamba  kwa sasa Watanzania wana hofu pamoja na hisia tofauti juu ya usalama wao hivyo ni vyema kukubali vyombo vya nje kufanya uchunguzi ili kupunguza hisia hizo.

"Kuomba msaada siyo fedheha. Msaada siyo jambo geni, kwa uzoefu wangu nilipokuwa Waziri  askari wengi walikuwa wanafanya 'training' nje naamini hata mpaka sasa. Tunapoomba msaada siyo kwamba haina uwezo bali inasaidia kuondoa hofu kwa wananchi. Ninachokuomba Rais waagize makamanda wako kuomba msaada ili Watanzania wasiishi kwa hofu" Masha.

Ameongeza kwa kusema kwamba "Tusikatae misaada, kwani hakuna aliyesema askari wa Watanzania siyo waadilifu japo wachache siyo. Siyo maisha yetu kukuta watu wamekufa ufukweni hofu kwa Watanzania hatujaizoea.

Pamoja na hayo Mh. Masha amekiri wazi kumshangaa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba pamoja na Inspekta Jenerali wa Tanzania Simon Sirro kwa kukataa msada wa kutoka nje wa kiuchunguzi ili kusaidia kupunguza hisia na hofu kwa Watanzania kwani ndiyo kazi ya jeshi la polisi.

Hata hivyo ameongeza na kutoa rai kwa serikali kwamba matukio hayo hayaathiri Watanzania tu kwani hata mataifa ya nje wanajiuliza kuhusu usalama wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment