Wednesday, 18 October 2017

Kamanda Mambosasa atoa tamko zito kuhusu wanaojiusisha na Ushoga.

Related image
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa, ametangaza vita na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wale ambao wanafanikisha kuwepo kwa vitendo hivyo, akisema kamwe hawatwaacha salama.

Kamanda Mambosasa ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, na kusema kwamba serikali hairuhuhusu kuwepo kwa vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na sheria za nchi, na pia jeshi la polisi litahakikisha linamkamata kila atakayegundulika kujihusisha navyo.

Kamanda Mambosasa ameyasema hayo kufuatia tukio la kukamatwa kwa meneja wa hoteli ya Peacock ambaye alitoa Ukumbi kwa ajili ya watu wanaofanya vitendo hivyo kufanya mkutano wao, pamoja na watu wengine ambao ni raia wa Afrika Kusini, Uganda na Tanzania.

“Tumekamata wahalifu wengine pale Peacock ambao wanahamasisha ushoga hapa nchini, niendelee kutoa onyo kwamba kosa hilo kwetu ni kinyume na sheria, kwanza meneja wa hoteli tumemkamata kwa sababu alikuwa anajua ndio maana akatoa ukumbi, lakini pia wahusika warudi kwao wakaendelee huko kama sheria zao zinaruhusu, lakini kwa hapa nchini na kanda maalum ninasema ni marufuku na yeyote atakayepokea, kuhifadhi na kuwezesha kitendo hicho hatutamuacha”, amesema Kamanda Mambosasa.

Watu hao waliokamtwa wamefikia 12, ambao ni watu wa Afrika Kusijini wawili, Mganda mmoja na Watanzania 9, na watafikishwa mbele ya sheria hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment