Monday, 30 October 2017

Kauli ya Zitto Kabwe kuhusu kuwomba CHADEMA waungane katika Uchaguzi wa Madiwani.

Image result for kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amevitaka vyama vingine vya upinzani ikiwemo CHADEMA, kuunganisha nguvu ili kuhakikisha wanaing'oa CCM kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani.


Zitto Kabwe ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa kampeni za kuelekea uchaguzi huo, na kusema kwamba wamegundua iwapo wataunganisha nguvu na kuachiana baadhi ya kata, watafanikisha kukitoa chama cha CCM, na hatimaye kutimiza malengo yao ya kushikilia kata hizo.

"Iwapo vyama vyote vya upinzani vikituachia sisi kugombea kata za Kijichi tutaishinda CCM, na iwapo sisi tukiwaachia kata ya Mbweni wataishinda CCM, tunaomba wenzetu tuweke nguvu ya pamoja, tushinde Kijichi na Salanga, tumefanya utafiti tumeona tuna nafasi kubwa ya kushinda Kijichi, tuna nafasi kubwa ya kugawa kura na wenzetu Mbweni”, amesema Zitto kabwe
Zitto Kabwe ameendelea kusema kwamba ...”Tunawaambia wenzetu kupitia nyie, tuna adui mmoja tu CCM, tuache majivuno, ushirikiane, na sisi tumeonyesha 'good faith' tumewaachia Mbweni, tunawaomba wa-extend hiyo good faith, na wakihitaji maada tutawasaidia, ili kwenye kata zote zinazofanya uchaguzi Dar es salaam CCM ishindwe”.
Hivi karibuni kunatarajiwa kufanyika chaguzi ndogo ndogo za madiwani katika maeneo mbali mbali nchini, kwa mujibu wa sheria na katiba za nchi.

No comments:

Post a Comment