Monday, 16 October 2017

Kigezo alichotumia Askofu kumfananisha Rais Magufuli na Robert Mugabe.



Askofu wa Jimbo Katoliki Zanzibar Agustino Shao, amefananisha Rais Magufuli na Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, kwa uwajibikaji na kukemea vitendo vya rushwa.

Kwenye taarifa iliyotolewa na Ikulu kwa vyombo vya habari, imeeleza kuwa Askofu Shao ameyasema hayo kwenye ibada ambayo ilihudhuriwa na Rais Magufuli visiwani Zanzibar kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph, na kusema kwamba Rais Mugabe alichukua hatua za kupigania maslahi ya Wazimbabwe na sasa hivi wananeemeka na matunda hayo, kitendo ambacho amedai Rais Magufuli anakifanya kwa sasa, na kuwataka watanzania kumuunga mkono.

"Hatutaweza kusema tunaimaliza rushwa wakati tunaendelea kuishi kwa kupata fedha ambazo hatujazifanyia kazi. Ni lazima tuishi machungu ya kuimaliza rushwa. Ni lazima tuishi machungu ya kuweka uadilifu katika utendaji wetu, tusipoishi maisha hayo tutaishi dunia mbili, dunia ya rushwa na dunia ya kujenga uchumi na uadilifu wa watanzania, " amesema Askofu Shao.
Related image
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.
katika salamu zake akimshukuru Askofu Shao kwa mahubiri mazuri, amewahakikishia Watanzania kuwa serikali itachukua hatua kupambana na rushwa kulinda rasilimali za nchi, na kuwataka Watanzania wote kuungana katika hilo.

No comments:

Post a Comment