Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Geofrey Mwashiuya, amesema kuwa anajipanga kila iwezekanavyo ili aweze kuwafunga Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, kesho Jumamosi ndani ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ili aweze kujiongezea nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.
Mwashiuya amesema kwamba, mchezo wao dhidi ya Simba atahakikisha anapambana vilivyo ili wawafunge na kama yeye akipata nafasi hatafanya makosa ya kutowafunga kwa sababu anaamini kuwa uwezo wake wa sasa kama atawafunga atajiwekea hazina kubwa ya kuitwa kikosi cha taifa.
“Nashangaa nimekuwa nikiambiwa nacheza vizuri sana lakini kila kinapoitwa kikosi cha timu ya taifa mimi siitwi sijui tatizo nini hapo, kutokana na hivyo nimejipanga vilivyo katika mchezo wetu dhidi ya Simba kuutumia kuonyesha uwezo wangu maana wengi wamekuwa wakipimwa katika mechi kubwa kama hizi na kuwafanya waitwe katika kikosi hicho,” alisema Mwashiuya.
No comments:
Post a Comment