Friday, 20 October 2017

Kocha mpya wa Simba FC aanza kwa kutoa kauli Tata.

Image result for Masoud Juma on Rayon Sports
Kocha mpya wa Simba, Irambona Masoud Juma amezua gumzo mtandaoni baada ya kusema kauli mbalimbali.

Kauli mbili za kuwa hatafunga begi lake na kama mabaya ataondoka zake mapema kurejea Kigali, Rwanda na ile wachezaji wavivu wajiandae, imewavutia watu wengi.

Kutokana na wengi kuvutiwa na kauli hiyo, wamekuwa wakijadili mambo kadhaa ikiwemo kuwachambua wachezaji wavivu.

Lakini baadhi wamekuwa wakieleza kufurahishwa na namna kocha huyo alivyoonyesha kujiamini hiku baadhi wakitaka viongozi na wachezaji wenyewe kumuunga mkono.

Kocha huyo kijana amejiunga na Simba akitokea nchini Rwanda ambako alifanya vizuri na Rayons Sports.

Kabla Masoud alikuwa mchezaji wa APR ya Rwanda ambako alifanya vizuri kabla ya kustaafu na kuwa kocha.

No comments:

Post a Comment