Monday 23 October 2017

Rais Magufuli awatunuku vyeti wajumbe wa kamati za Makinikia leo.


Image result for Rais Magufuli awatunuku vyeti wajumbe wa kamati za Makinikia leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Oktoba, 2017 atawatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni ya Banick Gold.

Tanzania na Barrick Gold Corporation zilifikia makubaliano tarehe 19 Oktoba, 2017 na kutiliana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika migodi yake hapa nchini, pamoja na kulipa takribani Dola za Marekani milion 300 za kuonesha nia njema ya kufidia madai ya upotevu wa mapato yaliyotokana na biashara hiyo.

Tukio hili litafanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 5:00 asubuhi na kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao mbalimbali.

Mkungenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU Dar es Salaam
23 Oktoba, 2017

IMG_20171023_093022.jpg

No comments:

Post a Comment