Kiungo nyota wa Simba, Shiza Kichuya amelia na viwanja vya mikoani kuwa ni chanzo cha wachezaji wengi kuwa majeruhi.
Kichuya ambaye hivi karibuniYanga inatarajiwa kuondoka kesho kwa ndege kwenda mkoani Kagera kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera.
Hivi karibuni, Kichuya alikuwa majeruhi kwa siku chache kabla ya kurejea uwanjani baada ya kupata matibabu.
"Mikoani inabidi ujiandae hasa unapoangalia ni suala la viwanja, kweli ni vibovu sana.
"Kama ni ushauri wavifanyie kazi kulinda afya zetu, ni hatari sana," alisema.
Simba ikiwa Kanda ya Ziwa, Kichuya alifunga moja ya mabao bora dhidi ya Stand United baada ya kupokea pasi nzuri ya John Bocco.
No comments:
Post a Comment