Baada ya kuwepo na taarifa za uhakika kuwa Simba imefanya mazungumzo na kumalizana na Kocha Masoud Juma raia wa Burundi, taarifa nyingine kutoka mjini Kigali zimeeleza, kocha huyo ameishawaaga rafiki na ndugu zake.
Imeelezwa Juma ambaye alipata mafanikio makubwa kama kocha akiwa na Rayon Sports ya Rwanda ameaga kuwa anasafiri kwenda Tanzania kuanza kazi yake mpya.
Kocha huyo anatua Simba kuwa mrithi wa Jackson Mayanja raia wa Uganda aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba.
Juma aliwahi kuwa mchezaji nyota wa APR ya Rwanda na anasifika kwa soka la nguvu na kasi.
No comments:
Post a Comment