Mshambuliaji wa Paris St-Germain Edinson Cavani, 30, anataka kujiunga na join Pep Guardiola klabu ya Manchester City baada ya kukorofishana na mchezaji mwenzake Neymar. (Don Balon, kupitia Manchester Evening News)
Kiungo wa kati wa Manchester United Juan Mata, 29, alikataa mshahara wa £375,000 baada ya kutozwa ushuru ambao alikuwa ameahidiwa iwapo angehamia Ligi Kuu ya China. (The Sun)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger alijibizana vikali na mwamuzi Neil Swarbrick baada ya timu yake kulazwa 2-1 na Watford Jumamosi na huenda akafunguliwa mashtaka na chama cha soka England, FA. (London Evening Standard)
RB Leipzig hawangemuuza Naby Keita kwa Liverpool isipokuwa tu ni kwamba kulikuwa na kifungu cha kumwachilia kwenye mkataba wake, klabu hiyo ya Ujerumani imesema. Keita, 22, atahamia Anfield majira ya joto yajayo baada ya Liverpool kukubali kulipa ada ya juu kufikisha kiwango cha kumfungua kutoka kwa mkataba wake cha £48m ambacho kitaanza kutekelezwa mwisho wa msimu huu. (Liverpool Echo).
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema hatastaafu akiwa bado katika klabu hiyo na amedokeza kwamba huenda akahamia Paris Saint-Germain ya Ufaransa akimaliza muda wake Old Trafford. (The Times)
Mourinho amesikitishwa na majadiliano ambayo yamejivuta kuhusu kuongezewa mkataba wake ambayo kufikia sasa yamefika katikati. (Daily Record)
Chelsea, Manchester City na Arsenal wanamfuatilia mshambuliaji chipukizi wa Barcelona wa miaka 17 ambaye kwa sasa anachezea klabu ya akiba ya Barca Abel Ruiz. Ada ya kumfungua kutoka kwa mkataba wake ni £3m. (Mirror)
Manchester City wanakusudia kuwasilisha ombi la kutaka kumnunua beki wa kushoto wa Southampton Ryan Bertrand, 28, mwezi Januari. (Daily Mail)
Barcelona waliwafuatilia wachezaji watatu wa Bayer Leverkusen Jumapili: Beki wa kati wa miaka 21 Jonathan Tah, winga Leon Bailey, 20, na winga Julian Brandt, 21. (Sport - kwa Kihispania)
Meneja wa West Brom Tony Pulis anaamini mkabaji Jonny Evans, 29, ameyumbishwa na hatua ya klabu kadha kutaka kumnunua majira ya joto yaliyopita. (Mirror)
Liverpool hawataruhusu mshambuliaji wao wa miaka 17 Rhian Brewster aende nje kwa mkopo Januari, lakini winga Lazar Markovic, 23, na beki wa kati Lloyd Jones, 22, wataruhusiwa kuondoka. (Sun)
Liverpool wanataka kumnunua kinda wa Fortuna Sittard kutoka Uholanzi Perr Schuurs, 17. (Daily Mail)
Barcelona huenda wakaamua kumgeukia kiungo wa kati wa Bayern Munich Thiago Alcantara, 26, iwapo watashindwa kumpata kiungo wa kati wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, Januari. (Don Balon kupitia Daily Express)
Villarreal wanataka sana kumnunua kiungo mshambuliaji wa miaka 17 anayechezea klabu ya America ya Mexico Diego Lainez. (ESPN - kwa Kihispania)
Lazio wanataka kumtuza beki Stefan de Vrij, 25, na mkataba mpya ili pia kuzuia klabu nyingine, hasa Liverpool, kumnyatia. (FourFourTwo)
Nottingham Forest wanaweza kujaribu kumnunua winga wa St Mirren na Scotland timu ya vijana wa chini ya miaka 21 Lewis Morgan, 21, ambaye pia amewavutia Celtic, Rangers na Birmingham City. (Daily Record)
No comments:
Post a Comment