Monday 16 October 2017

Orodha Mpya ya viwango vya FIFA Tanzania yazidi kuporomoka.

Related image
Shirikisho la soka duniani Fifa limetoa orodha mpya ya viwango vya soka duniani baada ya kuchezwa kwa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018, Kenya na Tanzania zikishuka zaidi ya hatua 10 kwenye orodha hiyo.

Ujerumani bado wanaongoza wakifuatwa na Brazil na Ureno.
Tanzania inashikilia nafasi ya 136 sasa baada ya kushuka nafasi 11, Kenya nayo imeshuka nafasi 14 hadi nafasi 102.
Katika mechi za kirafiki ambazo Harambee Stars walicheza hivi majuzi, walilazwa 1-0 na Thailand baada ya kuchapwa 2-1 na Iraq mjini Basra.
Burundi imesalia nafasi ya 129, Uganda ikapanda hatua moja hadi nafasi ya 70.
Malawi imeshuka nafasi moja hadi nambari 117 ambapo inafuatwa katika nafasi ya 118 na Rwanda ambao bado walishikilia nafasi hiyo katika orodha iliyotangazwa awali.
DR Congo wamepanda nafasi 7 hadi nafasi ya 35.
Afrika Tunisia wanaongoza wakiwa nafasi ya 28 duniani baada ya kupanda hatua 3 wakifuatwa na Misri walio nafasi ya 30 duniani.

Orodha ya Fifa
NafasiTaifa
1Ujerumani
2Brazil
3Ureno
4Argentina
5Ubelgiji
6Poland
7Ufaransa
8Uhispania
9Chile
10Peru
11Uswizi
12England
13Colombia
14Wales
15Italia
16Mexico
17Uruguay
18Croatia
19Denmark
20Uholanzi

No comments:

Post a Comment