Monday 6 November 2017

Ajibu atoa neno kwa mashabiki kuhusu Sare za Yanga

Related image
Yanga imepata sare ya pili mfululizo huku mashabiki wake wakionyesha kutofurahishwa baada ya kikosi chao kuomba mechi iishe mapema wakati Singida United walipokuwa wakishambulia kama nyuki.

Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba ikaonyesha soka safi na kuwapa presha Simba lakini presha hiyo ikaishia kwa Yanga baada ya mechi dhidi ya Singida United iliyoisha kwa sare ya 0-0, juzi.

Lakini mshambuliaji nyota wa Yanga, Ibrahim Ajibu, ameliona hilo, kwamba mashabiki hawafurahii hali hiyo na ametoa kauli yake.

Ajibu aliyejiunga na Yanga akitokea simba amesema  matokeo yasiyoridhisha wanayoyapata hivi sasa, ni sehemu ya mchezo, hivyo mashabiki waendelee kuwaunga mkono.

“Mashabiki watulie na waendelee kutuunga mkono ili tuweze kufanya vizuri kwenye mechi zijazo kwa sababu haya matokeo hata sisi hatuyafurahii.


“Matokeo yetu dhidi ya Singida ni sehemu ya mchezo, tulijitahidi sana kuhakikisha tunapata ushindi lakini haikuwa hivyo kwa sababu na wenzetu nao walijipanga, kikubwa ifahamike wazi kwamba, ligi bado mbichi,” alisema Ajibu.

Yanga na timu nyingine zina nafasi ya kujiandaa kwa kuwa kipindi hiki kutakuwa na mapumziko wakati wa kalenda ya Fifa, hivyo ni nafasi nyingine kuyafanyia kazi makosa ambayo yamekuwa yakijitokeza.

No comments:

Post a Comment