Wednesday, 1 November 2017

Kocha wa Simba FC Omog atoa ahadi juu ya Mchezo wao ujao na Mbeya City.

Image result for TIKISA MEDIA
Huku wikiendi hii kikosi cha Simba kikitarajiwa kuwa ugenini mkoani Mbeya, ambapo kitacheza mechi mbili, kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog ameweka wazi kuwa anataka kuvunja rekodi ambayo ni kuibuka na pointi sita kwenye michezo miwili mbele ya wapinzani wao, Mbeya City na Prisons.

Omog na jeshi lake la Simba litakuwa na kibarua kigumu cha kucheza kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambapo mara kwa mara wamekuwa na matokeo mabaya, ambapo Jumapili watawavaa Mbeya City kwenye uwanja huo kisha kumaliza na Prisons, Novemba 18, mwaka huu.

Mcameroon huyo amesema pamoja na rekodi mbaya kila wanapocheza uwanjani hapo lakini safari hii hawataruhusu hilo litokee kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa wa pointi tatu za kila mchezo.

“Tunajua kuwa mara kwa mara tunasumbuka kupata matokeo hapa Sokoine, lakini safari hii sitakubali kuona hilo linatokea tayari tumeshaweka mikakati kabambe ya kupata pointi sita kutoka kwa wenyeji wetu.

“Tunataka tushinde kwa ajili ya kujiongezea wigo wa pointi dhidi ya mahasimu wetu ambao tunalingana nao kwenye msimamo, na hatuwezi kuwakimbia bila ya kupata matokeo mazuri hasa kwenye mechi kama hizi za ugenini.

“Niseme wazi kwamba lile suala eti la kuwa na rekodi ya kupoteza mechi kila tunapokuwa hapa Mbeya kwa sasa ndiyo limefika mwisho,” alisema kocha huyo.


No comments:

Post a Comment