Wednesday, 1 November 2017

Niyonzima azungumzia jinsi yanga ilivyomtoa jasho.

Related image
KIUNGO wa Simba, Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda, amekiri ugumu kukutana na timu yake ya zamani ya Yanga kutokana na wapinzani wake hao kumjua vilivyo.


Simba na Yanga zilikutana wikiendi iliyopita katika mchezo wa ligi kuu ambao ulikuwa na upinzani wa hali ya juu ambapo matokeo yalikuwa bao 1-1, huku Simba ikiendelea kuongoza katika msimamo kufuatia kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Niyonzima alisema, mchezo ulikuwa na upinzani mkubwa hivyo anashukuru kwa matokeo waliyoyapata na kudai ilikuwa kazi kwa upande wake kutokana na kucheza na timu yake ya zamani ambayo inamjua vilivyo, lakini ataendelea kupambana kuisaidia Simba.

“Mechi ilikuwa na ushindani, kila upande ulikuwa ukipigana kuweza kupata pointi tatu, lakini tunashukuru kwa matokeo haya tuliyoyapata, tunaamini mwalimu atafanyia kazi upungufu uliojitokeza ili tuweze kufanya vyema katika mechi zijazo.

“Mchezo ulikuwa mgumu, siyo kazi rahisi kwangu kupambana na timu niliyoichezea miaka mingi, pia wananifahamu, lakini nimejitahidi kucheza kulingana na jinsi hali ilivyokuwa, kwani nilikuwa na upinzani mkubwa, nilipambana kucheza katika kiwango kizuri kulingana na hali ilivyo ingawa walinisumbua sana,” alisema Niyonzima.

No comments:

Post a Comment