Tuesday, 21 November 2017

Yanga yatoa msimamo wao kuhusu Donald Ngoma.

Image result for Donald Ngoma
Mshambuliaji Donald Ngoma ameendelea kubaki nchini Zimbabwe ambako inaelezwa amekwenda kwenye matibabu.

Yanga imeendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo bila ya kuwa na mshambuliaji huyo.

Tayari uongozi wa Yanga ulishalalamika kuhusiana na Ngoma kuondoka bila ya kuaga ingawa pia ilielezwa alimuaga kocha George Lwandamina.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alisema kwamba akirejea ataadhibiwa.

Pamoja na kuonekana anapendwa na mashabiki wa Yanga, lakini mara kadhaa Ngoma amekuwa akitajwa kwa utovu wa nidhamu katika klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment