Wednesday, 17 January 2018

Kocha wa Simba Djuma amuongelea Okwi na Mchezo wao na Singida United

Image result for kocha wa simba Masoud Djuma
Masoud Djuma (katikati)
Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma ametamka kuwa mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi anatarajiwa kuwepo kwenye orodha ya wachezaji atakaowatumia kesho mechi dhidi ya Singida United.

Hiyo, ikiwa ni siku moja tangu mshambuliaji huyo ajiunge na timu hiyo kwenye kambi ya pamoja ya maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida itakayochezwa kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Okwi amejiunga na kambi hiyo akitokea nyumbani kwao Uganda alipokwenda baada ya kuwa majeruhi.

Djuma alisema mshambuliaji huyo amerejea akiwa bado yupo fiti ambaye jana, asubuhi alifanya mazoezi ya nguvu ya pamoja na wenzake kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Singida.

Djuma alisema, mshambuliaji huyo amefanya mazoezi vizuri kwa kufanya programu zote za kukimbia mbio fupi na ndefu kabla ya kuchezea mpira.

Aliongeza kuwa, Okwi leo asubuhi atafanya mazoezi ya mwisho ya pamoja na wenzake kabla ya mchana kurejea jijini Dar es Salaam wakitokea Morogoro walipokwenda kuweka kambi ya kujiandaa na mechi dhidi ya Singida.

“Okwi amelirejea Dar Jumatatu na siku hiyo jioni alifika hapa mkoani Morogoro ambako tumeweka kambi kwa ajili ya mechi dhidi ya Singida tutakayocheza Jumatano.

“Mara baada ya kufika alifanya mazoezi ya pamoja na wenzake kabla ya  Jumatano asubuhi kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya timu kurejea Dar kwa ajili ya mechi dhidi ya Singida ambayo yeye anatarajiwa kuwepo kwenye orodha ya wachezaji nitakaowatumia, hakika naamini kuwa huyu ni mchezaji muhimu na ataisaidia sana timu hii,” alisema Djuma.

No comments:

Post a Comment