Thursday, 1 March 2018

Donald Trump apata pigo lingine katika Serikali yake

Image result for Hope Hicks with donald trump
Mkurugenzi wa mawasiliano na mmoja wa mashauri wa karibu wa Rais Trump wa muda mrefu ameachia ngazi yake,mamlaka imesema.

Mwanamke huyo wa miaka 29 aliyekuwa mwana mitindo na mfanyakazi wa kampuni ya Trump, amekuwa karibu naye kwa miaka mingi.
Anaripotiwa kuwaambia wafanyakzai wenzake kuwa amehisi ametimiza wajibu wake katika ikulu ya White House.
Yeye ni mtu wa nne aliyeshika nyadhifa wa mkurugenzi wa mawasiliano.
Image result for Hope Hicks

                       Hope Hicks

Msemaji wa White House Sarah Sanders amesema haijulikani ni lini haswa Bi Hicks ataondoka.
Amekanusha kuwa hatua hio inahusiana na ushahidi amabyo Bi Hicks aliutoa mbele ya kamati Congress wakati aliporipotiwa kukiri kusema uongo wa wazi kwa niaba ya Bw Trump.
Wakati wa kampeni za uchaguzi, Bi Hick alifanya kazi kama khatibu wa mawasiliano. Alichukua nafasi wa kuungoza idara ya mawasiliano ya White House Agosti iliopita, baada ya ufutaji kazi wa ghafla wa
Bw Anthony Scaramucci.
Kabla yake , Sean Spicer na Mike Dubke walishika nyadhifa hiyo.

No comments:

Post a Comment