Friday, 23 March 2018

Jose Mourinho atoa neno watu wanaoisema vibaya Manchester United

Related image
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema watu wenye "ubongo" na "fikira za kuelewa mambo ya msingi" wanafahamu na kuelewa kwamba klabu hiyo imo kwenye kipindi cha mpito.


Mourinho ameshutumiwa mara kwa mara kutokana na mtindo wake wa uchezaji ambao unadaiwa kutokuwa na ubunifu hata kidogo na pia kutoangazia uchezaji wa kushambulia.
Shutuma zilizidi baada ya United kuondolewa michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na klabu ya Sevilla ya Uhispania.
"Naelewa masikitiko ya kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, lakini sielewi kitu kingine chochote kamwe," Mourinho alisema alipokuwa anahojiwa na CNN.
"Katika historia ya soka kote duniani, na si England pekee, kila wakati umekuwa na klabu kubwa zaidi zikipitia kipindi cha mpito, na unakuwa na klabu nyingine kubwa zaidi zikiwa na vipindi vinavyoendelea vya ushindi kwa muda mrefu, na hizi huwa ni kama awamu katika klabu yoyote ile."
United, wamo nafasi ya pili Ligi Kuu ya Uingereza nyuma ya Manchester City lakini pengo kati yao ni alama 16.
City huenda wakatawazwa washindi wa ligi kwenye debi ya Manchester itakayochezewa uwanja wa Etihad mnamo 7 Aprili.

Romelu Lukaku and Jesse LingardHaki miliki ya picha
Image captionLukaku alifunga bao la kufutia machozi dakika za mwisho mechi yao dhidi ya Sevilla

Baada ya United kufuzu kwa nusu fainali Kombe la FA kwa mara ya 29 kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Brighton Jumamosi, Mourinho aliwashutumu wachezaji wake akisema "waliogopa kucheza" na pia akatilia shaka sifa zao kama wachezaji binafsi.
Mkesha wa mechi hiyo, Mourinho, ambaye ni meneja wa zamani wa Chelsea, alitoa hotuba ya dakika 12 kutetea kazi yake United.
Mourinho alikuwa ameshinda kombe ndogo la klabu bingwa Ulaya, Europa League na pia KOmbe la Ligi msimu wake wa kwanza akiwa United.
Katika mahojiano na CNN aliongeza: "Ukiangalia Ligi ya Premia tuko na timu moja, klabu moja ambayo imejiandaa vyema sana kutushinda kwa miaka kadha iliyopita, na tuna klabu 18 nyuma yetu. Klabu moja mbele yetu, na 18 nyuma yetu.
"Bila shaka, katika siku zijazo tungependa kuwa na klabu 19 nyuma yetu lakini huu ndio uhalisia, uhalisia kwa watu wenye ubongo, walio na uwezo wa kufikiria mambo ya kimsingi, walio na ufahamu kuhusu jinsi mchezo huu ulivyo, kwamba tuko katika kipindi cha mpito.
"Na kuwa katika kipindi cha mpito na bado kufanikiwa kutimiza kwa mfano yale tuliyoyatimiza msimu uliopita, kushinda vikombe, na kufanikiwa kutimiza yale tunayojaribu kuyatimiza msimu huu, ambayo ni kujaribu bado kushinda kombe na kujaribu kumaliza wa pili ... Nafikiri tuko katika nafasi nzuri."

No comments:

Post a Comment