Friday 6 May 2016

WHO yatoa msaada huu kwa Wizara ya Afya nchini

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ajili ya mkakati wa kutoa chanjo kwa wakina mama na watoto dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara hiyo, Dkt. Neema Rusibamaila, amesema kuwa msaada huo utasaidia kutolewa chanjo katika mikoa na halmashauri mbalimbali nchini.

Aidha, amebainisha kuwa kwa hivi sasa hata vile vituo ambavyo havikuwa na majokofu ya kuhifadhia chanjo yatapata majokofu hayo ili kusogeza huduma za chanjo karibu kabisa na wananchi kwani yatapelekwa katika wilaya ambazo hazikuwa na majokofu na wataanzisha vituo vipya vya chanjo.

Akikabidhi vifaa hivyo Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufalo Chatoro amkesema kuwa vifaa walivyotoa ni pamoja na majokofu 200 pamoja na vifaa vitumikavyo kwa ajili ya kutolea chanjo.

No comments:

Post a Comment