Friday 6 May 2016

Rais Dk.Magufuli atoa kauli hii kuhusu wanaoficha sukari nchini.

index

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema wafanyabiashara wote wanaoficha sukari ni wahujumu uchumi na ikipatikana sukari yao wananchi watagawiwa bure.
Rais Magufuli ameyasema hayo akiwa njiani kuelekea jijini Arusha akitokea Mkoani Dodoma ambapo alifanya shughuli mbalimbali zikiwemo za serikali na chama cha mapinduzi.

''Pamekuwa na tabia moja ya ajabu sukari inapokuwa ina 'expire' Brazili na maeneo mengine inapouzwa sukari wafanyabiashara wenye tamaa ya pesa wanakwenda huko wananunua wanatuletea kwenye mabegi tofauti baadaye tunapata magonjwa ya kila aina wala huwezi kujua yametoka wapi tunataka tudhibiti biashara hii''- Rais Magufuli.

Nimeagiza vyombo vya dola vifuatilie watakao bainika sukari hiyo tutaigawa bure kwa sababu wafanya biashara hao ni wahujumu uchumi.

''Kuna mmja amenunua pake Kilombero tani elfu tatu hataki kuzitoa pale na mwingine kule mbagala kaficha tani elfu nne nataka niwaambie wakaichukue wauze kwa bei kadiri walivyokuwa wamepanga kwa sababu serikali ya Magufuli haitawavumilia''- Rais Magufuli.

Aidha Rais amewataka watanzania kuendelea kumuunga mkono na serikali yake na kumwombea kwa kufanya hivyo hatawaangusha.

No comments:

Post a Comment