Friday 6 May 2016

Kauli ya serikali kuhusu Tatizo la ubakaji na ulawiti hii hapa

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe, amesema kuwa tatizo la ubakaji na ulawiti nchini Tanzania limefikia pabaya baada ya takwimu kuonyesha kuwa kwa kipindi miaka mitatu mfululizo kuna matukio 19 ya ubakaji na ulawiti nchini kila siku.
 
Akizungumza bungeni leo Mjini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu Mhe. Mwakyembe amesema kuwa matukio hayo 19 ni yale ambayo yanaripotiwa lakini kuna uwezekano kuwa na mengi zaidi ysiyoripotiwa kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

Mhe. Mwakembe amewataka wabunge washirikiane katika kutatua tatizo hilo ambapo amesema kwa mwaka huu pekee kwa kipindi cha miezi mitatu kati ya mwezi Januari kuna mashauri yanayo fikia 2,031.

Aidha, Mhe. Mwakyembe ameipongeza Mahamaka na kusema kuwa pamoja na uchache wao wameweza kuzikamilisha kesi 111 ambapo watuhumiwa 96 wameshafungwa na watuhumiwa 18 wameachiwa huru kwa kukosa ushahidi na bado kuna kesi 1,920 kwa miezi mitatu ambazo hazijakamilika.

Aidha, Mhe. Mwakyembe akitolea ufafanuzi kuhusu hoja ya adhabu ya kuhasiwa kwa wanaume watakaokutwa na hatia ya kubaka au kulawiti amewataka wabunge wawasilishe muswada huo wa sheria kwani sio jukumu la serikali kutunga sheria kama hizo.

No comments:

Post a Comment