Thursday, 22 March 2018

Mbwana Samatta atoa ya moyoni kuhusu TFF.

Image result for Mbwana Samatta TAIFA STARS
Kueleka mchezo wa kalenda ya FIFA ambao ni wa kirafiki kati ya Algeria dhidi ya Taifa Stars, Nahodha Mbwana Samatta amesema itakuwa ni kipimo kizuri.


Akizungumza na kituo cha Radio EFM kupitia kipindi cha Sports Headquarters, Samatta amesema analipongeza Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa kuchagua mechi hiyo.

Samatta ameeleza mechi hiyo itakuwa ni kipimo kizuri kwao kutokana na utofauti wa viwango uliopo baina ya timu hizo mbili kutofautiana kwa mbali.

Ameongeza kwa kushauri ifikie hatua waendelee kutafuta timu ambazo zinakuwa bora dhidi yao ili waweze kupata nafasi nzuri ya kujipima, tofauti na wanapokutana na zenye viwango vidogo ambazo hata wakishinda hawapandi kwenye ubora wa soka duniani. 

Katika ubora wa viwango vya soka duniani Tanzania imeshika nafasi ya 146 wakati Algeria ikiwa imeshika namba 60.

Taifa Stars itacheza mchezo wa leo dhidi ya Algeria kuanzia majira ya saa mbili kamili usiku.

No comments:

Post a Comment