Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, amesema kuwa tangu mchezo wao umalizike dhidi ya Al Masry katika Kombe la Shirikisho Afrika, hajapata usingizi mzuri.
Okwi ameeleza hayo kutokana na namna alivyokuwa akiuwazia mchezo huo na namna walivyoweza kupambana lakini wakashindwa kupata matokeo.
“Nimeumia sana kuona tunaondoshwa kwenye mashindano muhimu kama yale, mimi binafsi sikutegemea kutofaulu ila kwa kuwa mchezo wa mpira ndivyo ulivyo basi tumekubali kwani siku nyingine tutajipanga zaidi".
“Al Masry ni timu kubwa tunaiheshimu lakini kwa namna ambavyo tumepigana, kama kusingekuwa na matatizo ya refa kutubania, naamini leo hii tungekuwa tutaongea mambo mengine,” alisema Okwi mwenye mabao 16 katika Ligi Kuu" alisema Okwi.
Simba walishindwa kusonga mbele baada ya kulazimishwa matokeo ya bila kufungana kwenye Dimba la Port Said huko Misri, Jumamosi iliyopita, na kuondoshwa rasmi kwenye mashindano.
No comments:
Post a Comment