Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Simba katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana, Kocha wa Tanzania Prisons, Abdallah Mohamed, asema penati waliyopata si halali.
Simba walipata penati mnamo dakika ya 80 kipindi cha pili baada ya mshambuliaji wao, John Bocco kudondoshwa katika eneo la hatari akiwa katikati ya mabeki wawili wa Prisons.
Mohammed ameeleza kuwa penati ile haikuwa sahihi na Simba walipendelewa tu na Mwamuzi huku akidai hawakustahili kupewa
"Kakweli maamuzi ya penati kama ile hauwezi ukatoa, haikuwa sahihi, naweza kusema walipendelewa tu maana hawakustahili kuipata" alisema.
Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo huo yaliyotiwa kimiani na John Bocco pamoja na Emmanuel Okwi.
No comments:
Post a Comment