Wednesday 30 May 2018

Mtibwa Sugar afunguka walichopanga kufanya kwa Singida United.

Image result for mtibwa sugar vs singida united
Kikosi cha Mtibwa Sugar kinaondoka leo mjini Morogoro kuelekea jijini Arusha kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United utakaopigwa June 2 2018 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


Kuelekea mechi hiyo Msemaji wa kikosi hicho, Thobias Kifaru anaamini kuwa wataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kutamba wataifunga Singida.

Kifaru anaamini watapata nafasi hiyo akieleza kuwa maandalizi yao yameenda vizuri huku morali ikifana kwa wachezaji wa kikosi chao.

Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wadau jijini Arusha pamoja na pande za mikoa mingine ndani ya Tanzania, tayari maandalizi yake yameshakamilika haswa Uwanja na kinachosubiriwa ni mchezo kufanyika.

Aidha, Shirikisho la Soka Tanzania limemtangaza mgeni rasmi wa fainali hiyo kuwa atakuwa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe.


No comments:

Post a Comment