Thursday, 3 May 2018

Tazama viongozi wa Dini wakicheka wakati Mbunge wa Iringa Peter Msigwa akimsifia Rais Magufuli.

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amefagilia Rais  John Magufuli kwa juhudi zake za kuimarisha miundombinu ya uchumi ikiwemo miradi ya barabara na maji bila kujali majimbo yanayokaliwa na vyama vya upinzani.


“Msigwa amesema hayo jana Mei 2, 2018 baada ya uzinduzi wa barabara ya Ipogolo mkoani humo na kuongeza kuwa Rais Magufuli habagui vyama kama ambavyo huwa anasema kwamba ‘Maendeleo hayana vyama’. Mbunge huyo alienda mbele zaidi na kufafanua mambo ambayo Rais ameyafanya kwa Mkoa wa Iringa tangu aingie madarakani mwaka 2015.

“Mhe. Rais umekuwa ukisisitiza katika hotuba zako kuwa wewe hujali mambo ya vyama, na hii imedhirika kuwa kweli hujali vyama, umesaidia sana, hela za kutoka kwako zimekuja nyingi. Kama alivyosema Mhe. Mahiga, kuna barabara nzuri katika kipindi chako ambacho umekuwa Rais, umejenga barabara ya lami kutoka Mlandege mpaka kwa Mkuu wa Wilaya karibu Shilingi Bilioni 3.5.
“Tuna stendi nzuri ipo Ipogolo ya karibu Shilingi Bilioni 3, tuna maji, kwa hiyo kuna vitu vimefanyika kwa kweli Mhe. Rais hupendelei, hela zinakuja hata sisi ambao ni wa CHADEMA unaleta hela, kwa hiyo tunakupongeza sana,”  alisisitiza mbunge huyo.

BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO.

No comments:

Post a Comment