Thursday 7 June 2018

Kopcha wa Simba Pierre Lechantre awekwa njia panda.

Image result for Pierre Lechantre
Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre pamoja na Mwalimu wa viungo, Aimen Habib, kwa pamoja watakosekana katika benchi la ufundi wakati Simba ikicheza dhidi ya Kakamega HomeBoyz FC leo.


Katika orodha ya wachezaji na benchi la ufundi wa kikosi hicho iliyotoka punde inaonesha Kocha Msaidizi pekee, Masoud Djuma ndiye atakuwa anaiongoza Simba katika mchezo wa nusu fainali ya Super Cup huko Kenya.


Haijajulikana sababu ya za kukosekana kwa wawili hao ni zipi ingawa imekuwa ikielezwa wamekuwa hawana mahusiano mazuri na kocha Msaidizi wa kikosi hicho.


Hivi karibuni kumezuka taarifa zinazoeleza kuwa Lechantre anaweza akatimkia Cameroon kwa ajili ya kutegemea kibarua cha kuinoa timu ya taifa hilo baada ya kutuma maombi ya kuomba kazi.


Aidha taarifa za ndani pia zinaeleza Lechantre na Aimen inawezekana safari ya kuitumikia Simba inaweza ikaishia baada ya michuano ya Super Cup kumalizika.


No comments:

Post a Comment