Wednesday 8 May 2019

Kauli Askofu Josephat Gwajima kuhusu video wa picha za ngono zilizosambaa mtandaoni.


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini Tanzania, Josephat Gwajima amekanusha kuhusika na video ya ngono inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii.


Kwa mujib wa Gwajima, video hiyo imetengenezwa na aliowaita maadui zake ambao wanalenga 'kumnyamazisha'.

Akiongea na wanahabari kwenye viunga vya kanisa lake jijini Dar es Salaam, Gwajima amesema msimamo wake na maono juu ya nchi ndiyo yamefanya kusingiziwa kashfa hiyo.

"Watu wanafanya haya ili nikose sauti. Wanasema 'tumpige Gwajima ili anyamaze.'" amesema na kuongeza: "Hizi picha zinajaribu kunichafua, lakini hawawezi."

Gwajima, ambaye pia amekuwa pia kwa namna moja ama nyengine akihusishwa ama kuhusika na siasa amesema: "Uchaguzi unakuja mwaka kesho (2020) na wanajua nina nguvu, hawataki niwe na sauti yoyote."

Hata hivyo, Gwajima hakuwataja kwa majina hao aliowaita kuwa ni maadui zake.
Video hiyo inayodaiwa kuwa ni ya Gwajima inamuonesha akiwa faragha na mwanamke wakifanya tendo la ngono. Na mtu anayedhaniwa kuwa ni Gwajima ndiye alikuwa akiichukua video hiyo kwa kutumia kamera ya mbele ya kifaa ambacho hakionekani.


"Ni mwanaume gani ambaye mwenye akili zake timamu anayeweza kujirekodi wakati akifanya tendo la ndoa? Haingii akilini," amejitetea Gwajima na kuongeza, "Zile ni picha za kuunganisha. Wametumia picha yangu moja ya kifamilia nikiwa kifua wazi na kuunganisha na picha nyengine ili wanichafue."
"...mkono wa huyo mtu anayejichukua ile video ni mkubwa, ni mkono wa 'baunsa' sio huu mkono wangu mdogo."
 

Gwajima pia amewaambia wanahabari kuwa tayari amesharipoti tukio hilo kwa mamlaka husika na kusema anatumai mtu aliyechapisha picha hizo kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram atakamatwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Askofu huyo aliambatana na viongozi wenzake wa kanisa lake pamoja na mkewe ambaye ameeleza kuwa ana imani na mumewe.


"...mimi ni jasiri kama Simba. Ukweli naufahamu. Mume wangu ninamfahamu na ninamwamini. Mungu akiwa upande wetu hakuna wa kutushinda," amesema Bi Gwajima


No comments:

Post a Comment