Sunday 1 March 2020

Kauli ya Mbelgiji kuhusu Yondani wa yanga.

 
AKIMCHEZESHA kwa mara ya kwanza namba sita, Kocha Mkuu wa Yanga Mbelgiji Luc Eymael amefurahishwa na kiwango kikubwa alichokionyesha beki wake mkongwe, Kelvin Yondani.


Kauli hiyo aliitoa mara baada ya mchezo wa hatua ya 16 Bora ya Kombe la FA uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambao ulimalizika kwa Yanga kuifunga Gwambina FC ya Misungwi, Mwanza bao 1-0.

Kocha huyo katika mchezo huo, alimchezesha Yondani namba sita kama kiungo mkabaji nafasi inayochezwa na Mkongomani Papy Tshishimbi na Abdulaziz Makame.

  Luc alisema kuwa alimchezesha Yondani namba sita baada ya Tshishimbi kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata kwenye michezo iliyopita ya Ligi Kuu Bara.

Luc alisema alimtumia Yondani kucheza nafasi hiyo baada ya kumuona anaimudu katika mazoezi yake ya siku mbili za mwisho kuelekea pambano hilo la FA.

Aliongeza kuwa amepanga kuendelea kumtumia mkongwe huyo katika nafasi hiyo kama akiona anahitajika baada ya kuvutiwa na aina yake ya uchezaji ya kulinda na kuchezesha timu akisaidiana na Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.
“Nimpongeze Yondani kwa kucheza vizuri namba sita kwa mara ya kwanza tangu nimejiunga na timu hii, nimempanga kucheza nafasi hiyo baada ya kumuona ana kontroo nzuri, pia ukabaji wake.

“Katika timu ninataka kuwa na wachezaji wa aina hiyo wenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja ndani ya uwanja, hivyo niahidi kuendelea kumtumia Yondani katika michezo ijayo,” alisema Luc.

Kwa upande wake Yondani alipotakiwa kuzungumzia hilo alisema: “Mimi nina uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja ndani ya uwanja, labda nafasi ambayo itanishinda kucheza ni kipa pekee.

No comments:

Post a Comment