Waziri mkuu wa Uingereza Boris
Johnson amelala hospitalini katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya
afya yake kuzorota kutokana na virusi vya corona.
Bwana Johnson amemtaka waziri wa maswala ya kigeni Dominic Raab kumsaidia pale atakapoweza, msemaji alisema.
Waziri mkuu mwenye umri wa miaka 55 alilazwa katika hospitali ya St. Thomas akiwa na dalili kali za virusi vya ugonjwa huo siku ya Jumapili jioni.
Malkia amekuwa akiarifiwa kuhusu afya ya Johnson kulingana na kasri la Buckingham.
Viongozi mbalimbali duniani akiwemo rais Donald Trump na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamemtumia risala za heri njema bwana Johnson.
Mwandishi wa maswala ya kisiasa wa BBC Chris Mason alisema kwamba waziri mkuu alipatiwa oksijen baadaye siku ya Jumatatu mchana kabla ya kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Alisahamishwa kama hatua ya kuchukua tahadhari ili awekwe karibu na mashine ya kumsaidia kupumua , alisema mwandishi huyo.
No comments:
Post a Comment