Sunday 16 August 2020

Sevilla vs Manchester United nani kusonga mbele ?

 https://www.imageservera.com/uploadedimages/202008/Aug13/CR_Sevilla-Man-United-4747.jpg

Manchester United ina nafasi ya kuthibitisha kiwango cha makali yao chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer Jumapili katika nusu fainali ya Ligi ya Europa.

Kumekuwa na ishara nzuri lakini ushindi dhidi ya Sevilla na kuingia fainali ya Ligi ya Europa itakuwa italeta picha nyumbani kwamba timu hii itafika mbali.

Nafasi katika fainali dhidi ya Inter Milan au Shakhtar Donetsk ndio zawadi inayowasubiri.

Bila shaka Sevilla ilitawala katika mchuano dhidi ya Wolves.

Wakati wanacheza mchezo huo, Sevilla ilidhihirisha kuwa na mchezo imara na hilo likawa muhimu sana kwao.

Sasa basi, United inahitajika kuisitisha Sevilla isiwe na mchezo kama huo, na hapo wa kukodolewa machoni Ever Banega, ambaye alikuwa mwongozaji mzuri sana wa timu yake wakati wa mechi ya robo fainali na timu hiyo ikaibuka na ushindi.

Baada ya Raul Jimenez kukosa penalti, na Joao Moutinho na Ruben Neves wakakosa kupata kick kwasababu ya miondoko ya kijana Banega akiwa na mpira na ushirikiano uliokuwepo na timu yake. 

Sergio Romero ameshiriki mechi 9 kati ya 11 ya Ligi ya Europa lakini huenda Solskjaer akaamua kumuamini David de Gea katika kile ambacho ni moja ya kechi muhimu sana za msimu.

Sevilla imerejea ikiwa ngangari kabisa baada ya kiungo wa kati Nemanja Gudelj, ambaye alipatikana na ugonjwa wa COVID-19 akiwa anarejea kwenye mazoezi kujitayarisha kwa Ligi ya Europa kusafiri Ujerumani Alhamisi kufuatia kipindi cha kujitenga na kupimwa tena.

Waliiokuwa wachezaji wa Manchester City Jesus Navas na Fernando watakuwa miongoni mwa wachezaji wa kufungua mechi.

Sevilla imefika nusu fainali ya kombe la UEFA Ligi ya Europa mara tatu za nyuma na kupata ushindi kwa mara zote hizo.

Ole Gunnar Solskjær nae, ameshinda mechi 49 kati ya 89 alizosimamia Manchester United.

Ushindi wa mechi hii utamfanya kuwa kocha wa tatu kupata ushindi mara 50 katika mashindano yote ya historia ya klabu hiyo baada ya Ernest Mangnall (78) na José Mourinho (81).

Je nani ataona lango la mwengine?

 

No comments:

Post a Comment